CMT Logo
Skip to main content
+255 738 785 651
info@cmt.go.tz
  • MMM
  • Wasiliana Nasi
  • Mrejesho
    • ENGLISH
    • SWAHILI
    National Emblem of Tanzania

    JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA  ·  WIZARA YA FEDHA

    BARAZA LA MASOKO YA MITAJI
    CMT Official Seal
    Dira na DhamiraMajukumu
    Wajumbe wa BarazaSekretarietiMuundo wa Taasisi
    Taratibu za RufaaNyaraka za RufaaAda za HudumaFomu
    SheriaTaratibuKanuniMarekebishoMafunzo ya mtandaonimajarida
    Kesi zilizoamuliwaKesi zilizowasilishwa
    HabariNyarakaPicha
    e-Rufaa

    Navigation

    Kuhusu Sisi ▾
    Dira na DhamiraMajukumu
    Utawala ▾
    Wajumbe wa BarazaSekretarietiMuundo wa Taasisi
    Namna ya Kukata Rufaa ▾
    Taratibu za RufaaNyaraka za RufaaAda za HudumaFomu
    Machapisho ▾
    SheriaTaratibuKanuniMarekebishoMafunzo ya mtandaonimajarida
    Kesi ▾
    Kesi zilizoamuliwaKesi zilizowasilishwa
    Kituo cha Habari ▾
    HabariNyarakaPicha
    e-Rufaa
    1. Home
    2. Namna ya Kukata Rufaa
    3. Taratibu za Rufaa
    Utaratibu wa Rufaa

    Uwasilishaji wa Rufaa Mbele ya Baraza

    Mamlaka na Wigo wa Rufaa

    Kwa mujibu wa Kifungu 136G (2) cha Sheria ya Masoko ya Mitaji na Dhamana [Sura ya 79], Baraza litakuwa na mamlaka ya kusimamia masuala yahusuyo;

    1. Kutafsiri utekelezaji au kanuni zozote zinazosimamiwa na sheria hii
    2. Migogoro baina ya Mamlaka na soko lolote la hisa
    3. Migogoro baina ya Mamlaka na dalali yoyote wa masoko
    4. Migogoro baina ya madalali wa masoko na wateja wao
    5. Migogoro baina ya makampuni yaliyoko kwenye masoko ya hisa na mamlaka za usimamizi au masoko ya dhamana
    6. Mamlaka kukataa maombi ya leseni
    7. Mamlaka kuweka ukomo au vizuizi kwenye leseni
    8. Mamlaka kufungia au kufuta leseni
    9. Kukataa kuidhinisha dhamana kwenye soko la hisa
    10. Kufungia uuzaji wa dhamana kwenye soko la hisa
    11. Kuiondoa dhamana kwenye orodha rasmi ya soko la hisa
    12. Mgogoro mwingine wowote unaoweza kujitokeza wakati Mamlaka inapotekeleza wajibu wake kwa mujibu wa sheria hii.

    Baraza halitakuwa na mamlaka kwenye masuala ya kijinai.

     

    Utaratibu wa Dhamana

    1. Mtu yeyote ambaye hajaridhishwa na uamuzi wa Mamlaka au upande wowote kama ilivyoelekezwa chini ya Kanuni ya 7(1) ya Kanuni za Masoko ya Mitaji na Dhamana, Tangazo la Serikali Na. 649 ya mwaka 2023 anaweza kukata rufaa kwa Baraza ndani ya siki thelathini (30) kuanzia tarehe ambayo uamuzi ulifanyika.
    2. Utaratibu wa rufaa utaanza kwa kuwasilisha maelezo kwa maandishi kwa Msajili wa Baraza, yakielezea mgogoro husika kama ilivyoainishwa chini ya Kanuni ya 7(1).

     

    Tangazo la Nia ya Kukata Rufaa

    Mtu yeyote anayekusudia kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa Mamlaka anapaswa kuwasilisha tangazo la nia ya kukata rufaa ndani ya siku saba (7) kuanzia tarehe ya uamuzi kufanyika.

    Tangazo la nia ya kukata rufaa litapaswa kutimiza vigezo vifuatavyo:

    1. Libainishe kama rufaa hiyo inahusu uamuzi wote au sehemu mahususi za uamuzi
    2. Likamilishwe kwa kujaza Fomu Na. 1 ya CMT, kama ilivyoelekezwa kwenye Jedwali la Kwanza kwenye Kanuni
    3. Lisainiwe na mleta maombi au mwakilishi wake mwenye idhini
    4. Liwasilishwe kupitia nakala saba (7).
      1. Ada ya uwasilishaji wa tangazo la nia ya kukata rufaa itakuwa kama ilivyoainishwa kwenye Jedwali la Pili kwenye Kanuni.
      2.  Upande wowote unaojiunga kwenye rufaa utapaswa pia kulipa ada kama ilivyoainishwa kwenye Jedwali la Pili kwenye Kanuni.

     

    NYARAKA ZA RUFAA

    Uwasilishaji wa rufaa

    1. Utaratibu wa kukata rufaa kwa Baraza utaanza kwa kuwasilisha Maelezo ya Rufaa kwa Msajili wa Baraza ndani ya siku thelathini (30) tangu tarehe ya uamuzi wa Mamlaka unaokatiwa rufaa.
    2. Maelezo ya Rufaa yataandaliwa kwa kutumia Fomu Na. 2 ya CMT, kama ilivyoelekezwa kwenye Jedwali la Tatu kwenye Kanuni.
    3. Kila rufaa itapaswa kujumuisha viambatanisho vyote muhimu vitakavyofanikisha kushughulikiwa kwa rufaa.

    Nyaraka Muhimu

           4. Bila kuathiri Kanuni Ndogo ya 2, rufaa itapaswa kuambatanishwa na nyaraka zifuatazo;

           a) Nakala iliyoidhinishwa ya uamuzi wa Mamlaka

           b) Nakala iliyoidhinishwa ya mwenendo wa shauri lililoendeshwa na Mamlaka

           c) Nakala ya Tangazo la Nia ya Kukata Rufaa

           d) Maelezo ya Rufaa

        e) Nyaraka nyingine zozote mleta maombi atakazoona zina umuhimu katika kuhakikisha rufaa inasikilizwa kikamilifu bila   upendeleo.

        5. Katika kuzingatia Kanuni Ndogo ya 4(b), “mwenendo” si lazima ujumuishe vielelezo na viambatanishi vilivyowasilishwa wakati wa usikilizaji wa shauri kwenye ngazi ya Mamlaka.

    Baraza linaweza, kwa utashi wake, kuhitaji kuwasilishwa kwa vielelezo na viambatanishi vilivyoletwa wakati wa usikilizaji wa shauri na Mamlaka.

    Habari na Matukio Habari →
    news
    CMT | Ziara ya Mafunzo – Kanada
    Nov 30, 2025
    news
    CMT | ICBMED ya 4, 2025 | Gold Crest Hotel Mwanza | 25–27 No...
    Nov 29, 2025
    Matangazo Tazama Zaidi →
    Maonesho ya Nanenane 2025, Dodoma — Ushiriki wa Ba...
    Aug 5, 2025New
    Nafasi ya Baraza katika Utekelezaji wa Dira 2050 “...
    Jul 20, 2025New
    Kuanza kwa utoaji wa Huduma
    Aug 19, 2024New
    CMT logo
    BARAZA LA MASOKO YA MITAJI
    JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

    Baraza la Masoko ya Mitaji (CMT) ni chombo huru cha rufaa kilichoanzishwa chini ya Kifungu cha 136A cha Sheria ya Masoko ya Mitaji na Dhamana, Sura. 79. Ikiwa na makao yake jijini Dar es Salaam, Tanzania, Baraza lina jukumu muhimu katika kuhakikisha usawa, uwazi na ulinzi wa wawekezaji katika soko la fedha.

    Wasiliana Nasi

    S.L.P 1384, Ghorofa ya Kwanza, Jengo la Hazina Ndogo (Posta - Mtaa wa Madaraka), Dar es Salaam, Tanzania
    +255 738 785 651
    info@cmt.go.tz

    Tovuti Mashuhuri

    • Tovuti Kuu ya Serikali
    • Soko la Hisa la Dar es Salaam
    • Soko la Bidhaa Tanzania
    • Wizara ya Fedha
    • Ofisi ya Msajili wa Hazina
    • Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana - CMSA

    Anwani Muhimu

    • Barua pepe
    • Tender

    Eneo / Mahali

    📍
    Hazina Ndogo · Dar es Salaam
    Open in Google Maps ↗

    Office hours

    Mon – Fri8:00 AM – 4:00 PM
    SaturdayClosed
    Sunday & HolidaysClosed
    © 2026 CMT, Haki zote zimehifadhiwa. | Imesanifiwa, Imetengenezwa na Huendeshwa na Baraza la Masoko ya Mitaji
  • Ramani ya Tovuti |
  • Kanusho |
  • Sera ya Faragha |
  • Hakimiliki |
  • Vigezo na Masharti
  • Stay Connected

    Get updates on rulings, announcements, and capital markets insights.

    Subscribe to Newsletter

    Receive important updates directly in your inbox.

    We respect your privacy. No spam.