CMT Logo
Skip to main content
+255 738 785 651
info@cmt.go.tz
  • MMM
  • Wasiliana Nasi
  • Mrejesho
    • ENGLISH
    • SWAHILI
    National Emblem of Tanzania

    JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA  ·  WIZARA YA FEDHA

    BARAZA LA MASOKO YA MITAJI
    CMT Official Seal
    Dira na DhamiraMajukumu
    Wajumbe wa BarazaSekretarietiMuundo wa Taasisi
    Taratibu za RufaaNyaraka za RufaaAda za HudumaFomu
    SheriaTaratibuKanuniMarekebishoMafunzo ya mtandaonimajarida
    Kesi zilizoamuliwaKesi zilizowasilishwa
    HabariNyarakaPicha
    e-Rufaa

    Navigation

    Kuhusu Sisi ▾
    Dira na DhamiraMajukumu
    Utawala ▾
    Wajumbe wa BarazaSekretarietiMuundo wa Taasisi
    Namna ya Kukata Rufaa ▾
    Taratibu za RufaaNyaraka za RufaaAda za HudumaFomu
    Machapisho ▾
    SheriaTaratibuKanuniMarekebishoMafunzo ya mtandaonimajarida
    Kesi ▾
    Kesi zilizoamuliwaKesi zilizowasilishwa
    Kituo cha Habari ▾
    HabariNyarakaPicha
    e-Rufaa
    1. Home
    2. Kuhusu Sisi
    3. Majukumu
    Majukumu Yake

    Baraza la Masoko ya Mitaji (CMT) la Tanzania ni chombo maalumu na huru cha maamuzi kilichoundwa kuhakikisha kunakuwepo usawa, uwazi na ulinzi kwa wawekezaji ndani ya mfumo wa masoko ya mitaji. Majukumu yake ya msingi yana mamlaka ya kimahakama na kiusimamizi, yakizingatia uhalisia wa masoko ya kifedha unaobadilika mara kwa mara kutokana na mazingira ya sekta yenyewe.

     

    Majukumu ya Msingi ya Baraza la Masoko ya Mitaji

      1. Utatuzi wa Migogoro   

    Baraza linatolea maamuzi migogoro inayojitokeza chini ya Sheria ya Masoko ya Mitaji na Dhamana [Sura ya 79], ikiwemo;

    • Migogoro baina ya Mamlaka na masoko ya hisa au madalali wa masoko
    • Migogoro baina ya madalali na wateja wao
    • Mivutano inayohusisha kampuni zilizopo kwenye masoko ya hisa, mamlaka za usimamizi, au masoko ya dhamana
    • Rufaa dhidi ya maamuzi yahusuyo leseni, kusitishwa kwa uuzaji wa hisa, au kuorodheshwa kwa dhamana

     

      2. Kutafsiri Sheria

    Baraza hutafsiri sheria na kanuni zinazohusu masoko ya mitaji, likitoa ufafanuzi wa kimamlaka juu ya vifungu vinavyosimamia uendeshaji wa masoko hayo.

      3. Mfumo wa Rufaa

    Baraza ndiyo jukwaa la msingi la maamuzi kwa pande zisidhoridhishwa na maamuzi ya Mamlaka. Linatoa utaratibu wenye mpangilio:

    • Kuwasilisha Tangazo la Nia ya Kukata Rufaa ndani ya siku saba (7) tangu uamuzi ufanyike
    • Kuwasilisha Maelezo ya Rufaa yaliyokamilika ndani ya siku thelathini (30) tangu uamuzi ufanyike.

     

      4. Ulinzi kwa Wawekezaji

    Kupitia utatuzi wa migogoro wenye ufanisi na uwazi, Baraza linalinda haki za wawekezaji na kukuza imani kwenye masoko ya fedha ya Tanzania.

     

      5. Mamlaka ya Kimahakama

    • Baraza lina mamlaka sawa na Mahakama Kuu, ikiwemo;
    • Kuita mashahidi
    • Kuapisha
    • Kuamuru upatikanaji wa nyaraka
    • Kutoa maamuzi ya mwisho kwenye masuala ya msingi (yanayoweza kukatiwa rufaa kwa kufuata vifungu husika vya sheria tu).

    Nafasi ya Kimkakati katika Uadilifu kwenye Masoko

    Baraza lina umuhimu kwenye Dira ya Taifa ya Maendeleo (Dira 2050), likichangia katika;

    • Utawala bora
    • Ufafanuzi wa sheria
    • Ukuaji endelevu wa kiuchumi
    • Uongozi kikanda kwenye utoaji wa maamuzi kwenye masuala ya masoko ya dhamana
    Habari na Matukio Habari →
    news
    CMT | Ziara ya Mafunzo – Kanada
    Nov 30, 2025
    news
    CMT | ICBMED ya 4, 2025 | Gold Crest Hotel Mwanza | 25–27 No...
    Nov 29, 2025
    Matangazo Tazama Zaidi →
    Maonesho ya Nanenane 2025, Dodoma — Ushiriki wa Ba...
    Aug 5, 2025New
    Nafasi ya Baraza katika Utekelezaji wa Dira 2050 “...
    Jul 20, 2025New
    Kuanza kwa utoaji wa Huduma
    Aug 19, 2024New
    CMT logo
    BARAZA LA MASOKO YA MITAJI
    JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

    Baraza la Masoko ya Mitaji (CMT) ni chombo huru cha rufaa kilichoanzishwa chini ya Kifungu cha 136A cha Sheria ya Masoko ya Mitaji na Dhamana, Sura. 79. Ikiwa na makao yake jijini Dar es Salaam, Tanzania, Baraza lina jukumu muhimu katika kuhakikisha usawa, uwazi na ulinzi wa wawekezaji katika soko la fedha.

    Wasiliana Nasi

    S.L.P 1384, Ghorofa ya Kwanza, Jengo la Hazina Ndogo (Posta - Mtaa wa Madaraka), Dar es Salaam, Tanzania
    +255 738 785 651
    info@cmt.go.tz

    Tovuti Mashuhuri

    • Tovuti Kuu ya Serikali
    • Soko la Hisa la Dar es Salaam
    • Soko la Bidhaa Tanzania
    • Wizara ya Fedha
    • Ofisi ya Msajili wa Hazina
    • Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana - CMSA

    Anwani Muhimu

    • Barua pepe
    • Tender

    Eneo / Mahali

    📍
    Hazina Ndogo · Dar es Salaam
    Open in Google Maps ↗

    Office hours

    Mon – Fri8:00 AM – 4:00 PM
    SaturdayClosed
    Sunday & HolidaysClosed
    © 2026 CMT, Haki zote zimehifadhiwa. | Imesanifiwa, Imetengenezwa na Huendeshwa na Baraza la Masoko ya Mitaji
  • Ramani ya Tovuti |
  • Kanusho |
  • Sera ya Faragha |
  • Hakimiliki |
  • Vigezo na Masharti
  • Stay Connected

    Get updates on rulings, announcements, and capital markets insights.

    Subscribe to Newsletter

    Receive important updates directly in your inbox.

    We respect your privacy. No spam.