+255 738 785 651
info@cmt.go.tz
Baraza la Masoko ya Mitaji ni maalumu kwa ajili ya kukuza uelewa, uwazi na utambuzi wa taratibu za kimfumo kwenye masoko ya mitaji nchini. Kupitia jukumu lake la kutoa muongozo, Baraza linawezesha uwepo wa muelekeo wa kimamlaka kwenye masuala ya kisheria na usimamizi yanayohusu washirika wa masoko, wawekezaji na taasisi.
Tunatoa muongo kwa:
Utoaji wetu wa miongozo unasaidia mfumo wa kisheria kueleweka, kupunguza wasiwasi na kuwawezesha wadau kushiriki kikamilifu kwenye masoko ya mitaji nchini. Iwe unaandaa rufaa, unatafuta leseni au unahitaji uelewa juu ya usimamizi wetu wa sheria, Baraza liko maalumu kwa ajili ya kuwezesha maamuzi sahihi na kuhakikisha kanuni za usawa na urahisi katika shughuli za masoko ya mitaji zinafuatwa.